Wednesday, 26 August 2015

AMANI YA TANZANIA

 AMANI YA TANZANIA
Jibu ni moja tu ni UPENDO na UVUMILIVU.

Watanzania wanatakiwa kuendeleza na kuimarisha upendo baina yao. Kwakuwa panapo upendo hakuna unyonyaji wala ukandamizaji achilia mbali vita.
Upendo unaanzia ngazi ya chini kabisa ambayo nafsi ambayo hukaa ndani ya familia. Kila nafsi ikiwa na upendo Dunia imekuwa na amani.
Ndio maana familia ikiwa na upendo inaishi kwa amani na hiovyo hivyo upendo huo utaingia mpaka kwenye muundo wa  masuala mbalimbali ya kijamii kama vile vyama vya siasa.
Uchafu wa viongozi wetu na watu wetu inaonyesha kuwa jamii yetu na familia zetu ni chafu kwakuwa hawa watu ni ndugu zetu tunaoishi katika jamii moja na uchafu wao unaonyesha nafsi zetu na familia zetu zilivyo.
kwamba watu wote na familia zote za Tanzania zinahimiza ufisadi, uchu wa madaraka, na matendo yote maovu lasivyo hawa watu hizi tabia wamezipata wapi kama si kwa jamii iliyowalea.
mtu mzuri au mbaya anatengenezwa na familia na familia zinatengeneza jamii; Hivyo basi mtu fisadi ametengenezwa na jamii ya kifisadi na kinyume chake ni kweli.
Ninadhani kuna haja ya amani kuanza kuhubiriwa kwanza kwenye mizizi (familia),  familia zetu zitengeneze watu tunaowahitaji kama jamii ili tuweze kupata jamii tunayoitaka.
Amani ni matokeo ya upendo.

Mungu Ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment