AMANI YA TANZANIA
Jibu ni moja tu ni UPENDO na UVUMILIVU.
Watanzania wanatakiwa kuendeleza na kuimarisha upendo baina
yao. Kwakuwa panapo upendo hakuna unyonyaji wala ukandamizaji achilia mbali
vita.
Upendo unaanzia ngazi ya chini kabisa ambayo nafsi ambayo
hukaa ndani ya familia. Kila nafsi ikiwa na upendo Dunia imekuwa na amani.
Ndio maana familia ikiwa na upendo inaishi kwa amani na
hiovyo hivyo upendo huo utaingia mpaka kwenye muundo wa masuala mbalimbali ya kijamii kama vile vyama
vya siasa.
Uchafu wa viongozi wetu na watu wetu inaonyesha kuwa jamii
yetu na familia zetu ni chafu kwakuwa hawa watu ni ndugu zetu tunaoishi katika
jamii moja na uchafu wao unaonyesha nafsi zetu na familia zetu zilivyo.
kwamba watu wote na familia zote za Tanzania zinahimiza
ufisadi, uchu wa madaraka, na matendo yote maovu lasivyo hawa watu hizi tabia
wamezipata wapi kama si kwa jamii iliyowalea.
mtu mzuri au mbaya anatengenezwa na familia na familia
zinatengeneza jamii; Hivyo basi mtu fisadi ametengenezwa na jamii ya kifisadi
na kinyume chake ni kweli.
Ninadhani kuna haja ya amani kuanza kuhubiriwa kwanza kwenye
mizizi (familia), familia zetu zitengeneze
watu tunaowahitaji kama jamii ili tuweze kupata jamii tunayoitaka.
Amani ni matokeo ya upendo.
Mungu Ibariki Tanzania